Archive for the ‘Jinsi ya kuweka viungo’ Category

Jinsi ya kuweka kichwa cha viungo na viungo

February 5, 2006

Ingia ndani ya blogu yako, kisha bonyeza kwenye kidude kisemacho “change settings.” (kidude hicho ni cha rangi ya bluu, kiko kama tairi la trekta. [tazama mchoro hapo chini]). Ukishabonyeza hapo nenda sehemu iitwayo TEMPLATE. Template (templeti) ndio ukurasa wenye maelezo yanayounda muundo na muonekano wa blogu uliyochagua ulipofungua blogu yako. Kidude cha kukupeleka ndani ya templeti yako kiko juu kabisa pamoja na na vidude visemavyo Posting, Settings, na View Blog. Bonyeza kwenye kidude cha Template ambapo utapalekwa kwenye ukurasa wenye maelekezo ya kifundi (kodi za kuunda kurasa za tovuti za HTML) juu ya blogu yako. Unaweza kuweka viungo vya blogu au tovuti mbalimbali chini ya maelezo yako binafsi (profile). Ukishaona kodi za maelezo binafsi zinapoishia, unaweza kubandika kodi za viungo vya blogu au tovuti .

Blog Name

New Post

Change Settings

Last Update

Posts

Create new post

HAPA PATAKUWA NA JINA LA BLOGU YAKO

Create new post (bonyeza hapa) Change blog settings 05 Feb 2006 0

Utakapoona sehemu muafaka ya kuweka viunganishi,tumia kodi na maelezo ambayo utapata ukibonyeza hapa.

Advertisements