Archive for the ‘Jinsi ya kuandika jambo’ Category

Jinsi ya kuandika jambo kwenye blogu yako

February 5, 2006

Kwa sasa maelezo ya jinsi ya kuandika jambo kwenye blogu yako yanahusu huduma ya blogu ya http://blogspot.com ambayo ndio inatumiwa na wengi kwa sasa.  Ingawa ina mapungufu yake, bado ina urahisi fulani hasa kwa watu wanaoanza.  Baadaye nitaandika maelezo ya huduma nyingine hasa WordPress ambayo ni programu huria.  Kwahiyo ili kufuatana nami katika maelezo haya itakupasa ufungue blogu kupitia: http://blogspot.com
Ukishafungua blogu yako, kinachofuata ni kuandika unayotaka. Tembelea blogu za wengine ili kupata picha ya mambo ambayo unaweza kuwa unaandika. Ili uandike jambo, ingia kwenye blogu yako kwa kutumia neno lako la siri. Ukishaingia bonyeza pale pasemapo: New Post (penye alama ya msalaba wa kijani [Tazama mchoro hapo chini]). Ukishabonyeza hapo utapelekwa kwenye sehemu ambayo itakuwa na kisanduku cha kuandika kichwa cha habari yako na pia sehemu ya kuandika unayotaka.

Blog Name

New Post

Change Settings

Last Update

Posts

Create new post

HAPA PATAKUWA NA JINA LA BLOGU YAKO

Create new post (bonyeza hapa. patakuwa na msalaba wa kijani) Change blog settings 05 Feb 2006 0
Advertisements