Archive for the ‘Huduma za bure za Blogu’ Category

Kati ya Blogger na WordPress ipi bora?

February 19, 2006

Baadhi ya wasomaji kwenye blogu yangu wametaka kujua zaidi kuhusu huduma za kublogu za Blogger na WordPress. Nimelinganisha huduma hizo katika makala ambayo utaisoma kwa kubonyeza hapa kwanza kisha bonyeza hapa.

Advertisements

Huduma za Blogu za Bure

January 16, 2006

Unapotaka kublogu swali la kwanza la kujiuliza ni kuhusu huduma utakayotumia. Zipo huduma nyingi sana hivi sasa zinazowezesha watu kufungua blogu zao kwa urahisi.  Zipo huduma za bure na nyingine za kulipia. Kwakuwa mwongozo huu ninaulenga zaidi kwa wazungumzaji wa Kiswahili walioko barani Afrika, nitaweka orodha ya hduma za bure.  Kwanza, tunajua matatizo ya kipato barani Afrika na pia watu wachache sana wanaweza kulipia huduma za malipo kwa kutumia kadi.  Hduma nyingi za malipo zinahitaji uwe na kadi ya benki au kadi nyingine kama vile VISA au Mastercard.  Kwa sasa huduma za bure zilizopo zinakidhi kwa kiasi kikubwa mahitaji ya wanablogu.  Sisemi kuwa huduma hizi hazina mapungufu.  Yapo mapungufu katika huduma hizi, kwa mfano lugha.  Lugha yetu bado haijatambulika kwa watengeneza programu hizi.  Mapungufu haya yanatafutiwa dawa.  Rafiki yangu Chris wa Progressive ICT Review na mimi tunatengeneza programu ya kublogu ambayo itakuwa ni dawa ya mapungufu ambayo yapo katika huduma za bure zilizopo hivi sasa. Wanablogu wa Tanzania karibu wote wanatumia huduma za blogger (http://www.blogger.com). Moja ya mambo muhimu ya kufanya wakati wa kutafuta huduma kwa ajili ya blogu yako ni kutembelea blogu za wengine.  Kwa mfano, ukibonyeza hapa utaona blogu mbalimbali za Watanzania.  Ukibonyeza hapa utaona blogu mbalimbali za Wakenya (Wakenya wanatumia huduma mbalimbali ikiwemo ya “blogger” na nyingine za kulipia).  Maelezo ya jinsi ya kufungua blogu zako katika huduma nitakazoorodhesha hapo chini sio magumu kufuata. Ila mwongozo huu kwa sasa utakuwa unalenga zaidi watumiaji wa huduma za “blogger” ambazo ndio Watanzania wengi wanatumia kwa sasa. 

Orodha ya Huduma za Bure:

  1. http://www.blogger.com
  2. http://www.wordpress.com
  3. http://www.livejournal.com/
  4. http://www.blog.co.tz/
  5. http://theblogs.net/
  6. http://www.ebloggy.com/
  7. http://www.blogsome.com/