Scoopt: Huduma Poa Kwa Wanablogu wa Picha na Wapiga Picha

Iwapo wewe ni mwanablogu wa picha au mpiga picha na ungependa uwe unauza picha zako, kuna huduma inaitwa Scoopt. Huduma hii inachofanya ni kutafuta vyombo vya habari ambavyo vitanunua picha yako kisha mnagawa mapato nusu kwa nusu. Wewe asilimia 50 na wao 50. Mchezo umekwisha. Ila picha zenyewe lazima ziwe zinauzika na sio picha za familia yako, mbwa wako, majirani wako, n.k. Bonyeza hapa utembelee tovuti ya Scoopt. Ukitaka kujua aina ya picha ambazo wanazipenda, bonyeza hapa.

Iwapo unatumia huduma ya Flickr kuhifadhi picha zako, na ungependa jamaa wa Scoopt wazipate picha zako, unashauriwa kutumia neno “scoopt” kama neno la kuashiria maudhui ya picha yako (kwa kiingereza “tag”).

Advertisements

3 Responses to “Scoopt: Huduma Poa Kwa Wanablogu wa Picha na Wapiga Picha”

  1. Jikomboe » Tumia Scoopt, Synthasite, na Snap Says:

    […] Kama wewe ni mpiga picha au mwanablogu wa picha, bonyeza hapa usome jinsi utakavyoweza kuuza picha zako. Kwa wale wanaopenda kujenga tovuti zao wenyewe ila hawana ujuzi au muda wa kujifunza toka A hadi Z, bonyeza hapa. Kisha kama wewe ni mwanablogu na unapenda kutumia huduma inayopiga picha tovuti au blogu ambazo umeweka viungo vyake katika mambo unayoandika (kama unavyoona inavyokuwa katika viungo nilivyoweka hapa), bonyeza hapa. Hizi zote ni makala fupi mpya nilizoweka kwenye Mwongozo wa Wanablogu.   […]

  2. Jikomboe » Filamu: Kenya’s Mobile Revolution + You Witness News Says:

    […] niliandika kuhusu iReport na pia niliwahi kuandika kwenye mwongozo juu ya Scoopt (ambapo wapiga picha wanaweza kuuza picha zao). Yahoo! nao wana mradi uitwao You Witness News […]

  3. Benitus Bonifas Says:

    nini maana ya dtt

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s


%d bloggers like this: