Huduma za kuhifadhi makala ndefu na Jinsi ya kuweka makala bloguni

Iwapo unaandika makala ndefu (waandishi wa habari hupenda kuita makala ndefu “mikeka”) au labda wewe ni mwanasafu na unapenda kuweka makala zako kwenye blogu yako, zipo huduma kadhaa ambazo unaweza kutumia ili kuhifadhi makala hizo. Kisha utanakili anuani ya makala zako toka kwenye huduma uliyotumia na kubandika kwenye blogu yako. Msomaji akibonyeza ulipoweka kiungo cha makala hiyo ataweza kuisoma. Huduma hizi ni za bure (zipo pia za kulipia ila nadhani hakuna sababu za msingi za kuacha kutumia huduma hizi za bure).

Huduma zenyewe:

1. Ripway: http://www.ripway.com

Huduma hii inatumiwa na wanablogu wengi wa Kiswahili. Huduma hii ni nzuri ingawa ina kiwango cha ukubwa wa mafaili ambayo unaweza ukahifadhi hapo. Unaweza kuhifadhi makala zenye ukubwa wa 30MB (jumla ya makala zote). Utahitaji kuwa na makala nyingi na ndefu sana kuweza kufikia kiwango hicho kwa haraka. Ukifikia kuwa na makala za ukubwa huo unaweza kuanzisha akaunti mpya kwa jina jingine! Pia kuna kiwango cha ukubwa wa mafaili ambayo yanaweza kusomwa katika kipindi cha masaa 24 ambayo ni 15MB. Wasomaji wakisoma makala zenye ukubwa zaidi ya huo akaunti yako itasimama kwa muda (baadaye itaendelea kufanya kazi).

Muhimu: usipoitumia akaunti yako katika kipindi cha mwezi mzima itafungiwa kwa muda. Hivyo lazima uwe unaingia ndani ya akaunti hiyo (hata kama huna makala mpya za kuweka) mara kwa mara.

2. Box: http://www.box.net/

Huduma ya Box inakuwa nafasi kubwa zaidi ya Ripway ya kuhifadhi makala au hadithi zako. Una nafasi ya ukubwa gigabaiti 1 (IGB) bure. Ukitaka nafasi zaidi itabidi ulipie. Huduma hii inakuwezesha kubandika kiungo cha makala au hadithi yako kwenye blogu yako kwa ajili ya wasomaji wako.

3. Freefilehosting: http://www.freefilehosting.org/

Freefilehosting wanakupa nafasi ya ukubwa wa 50MB na pia kiungo cha makala ulizohifadhi ili uweze kuweka kwenye blogu yako.

4. Gimehost: http://www.gimehost.com/

Huduma ya Gimehost, ingawa haijajengwa vizuri kama Ripway inaweza kuchukua makala zako utakazoandika maisha yako yote, Yaani hakuna ukubwa wa mafaili ambao ndio kikomo. Pia wasomaji wanaweza kusoma makala zako bila kuzuiwa pale watakapokuwa wamesoma makala za ukubwa fulani. Huduma hii inakupa kiungo ambacho utakiweka kwenye blogu yako.

Jinsi ya kuweka kiungo cha makala kwenye blogu yako:

Ukishachagua huduma unayotaka, ukapandisha makala, utapewa kiungo/anuani ya webu. Nakili kiungo/anuani hiyo kisha ingia ndani ya blogu yako.

Kama unataka kuwa na kona maalum ya makala zako kwenye ufito wa pembeni (sidebar) itabidi ujue jinsi ya kuweka kichwa cha habari cha kona za makala zako. Maelezo hayo hapo chini:

<h2 class=”sidebar-title”> HAPA WEKA KICHWA/JINA LA KONA YA MAKALA ZAKO</h2>

* Weka jina la makala yako katikati ya alama: > na < (kama ilivyo hapo juu).

Halafu jinsi ya kuweka makala zenyewe kwenye ufito wa pembeni (sidebar), yaani chini ya jina la kona yako ya makala. Utachukua anuani/kiungo ulichopata toka kwenye huduma ya kuhifadhi makala (nilizozielezea hapo juu) na kuweka katikati ya alama za kufungua na kufunga usemi kama ilivyo hapo chini:

<ul>

<li><a href=”HAPA UTAWEKA ANUANI/KIUNGO CHA MAKALA YAKO”>HAPA UTAWEKA KICHWA CHA MAKALA YAKO AMBACHO NDIO KITAONEKANA KWA WASOMAJI KWENYE BLOGU</a></li>

</ul>

Kwahiyo kila utakapokuwa unaweka makala itabidi utumie muundo huo hapo juu. Jambo la kuhakikisha ni kuwa makala zote lazima ziwe katikati ya alama <ul> na </ul>. Hizi ndio “code” za kufunga na kufungua kwahiyo mambo yote weka hapo katikati.

Mahali pa kuweka ndani ya blogu: itabidi uingie ndani ya blogu kwa kutumia neno lako la siri. Kisha nenda panaposema: “change setting”, halafu bonyeza kwenye “template.” Kisha ndani ya templeti tafuta sehemu ambayo utapenda kuweka kona ya makala zako. Templeti zinatofautiana na kila mtu ana upenzi wake wa eneo analotaka kuweka makala. Ila ni vyema ukaweka chini ya “code” zinazoweka kisehemu cha maelezo binafsi (profile). Popote chini ya hapo ni sawa.

Ukiwa na swali usisite kuniuliza: ughaibuni@yahoo.com au kumuuliza mwanablogu mwingine yeyote aliyebobea.

Advertisements

3 Responses to “Huduma za kuhifadhi makala ndefu na Jinsi ya kuweka makala bloguni”

 1. メル友募集掲示板 Says:

  よろしくおねがいします。good good nice

 2. HD Mavoice Says:

  Kwasasa nina nyimbo tatu ambazo azijafanyiwa production but kuanzi mwakani ngoma kama mbili zikuwa sokoni,kwa hiyo najitahind kumake mashairi makali maana nafanya hip pap but naipenda naninaielewa.kwahiyo sinabtdi kumake mashairi mazuri,mimi own naji

 3. HKiller"kisogo Says:

  KUTENGEZA BLOGS KUNAKUBIDI UWE SILIASI MAANA KUNA VITU VINGI SANA,,Duh nafanya mautundu mpaka mtaandao wa facebook unanipongeza. hatari charii full mashamushamu kama binti aliyeambia yeye ni mke mtalajiwa wa sam wa ukweli, wakati alikua akitoka na waziri,nihatari,
  kuna mambo mengi sana kwenye mitandao kujichanganya unainter kwenye nyavu, web site yako ina maana sawa na yangu andika mistari kila mtu akukubali, wasema kumbe dogo mwenye vipaji ni hatari kwenxe mashairi. poa sana wadau,,,nina mdogo wangu anaimba kama dangote, sijuhi anamuiga au ndo alivyo, poa sana hussein,aka h chozi, kuna pia na mjanja onlize aka onesmo dogo wa sebene,,,au sio mazee,

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s


%d bloggers like this: