Jinsi ya kutangaza blogu yako

Baada ya kufungua blogu ni muhimu sana kutumia njia mbalimbali za kuitangaza ili ujumbe wako uweze kufikia watu wengi. Kati ya njia unazoweza kutumia ni kusajili blogu yako kwenye tovuti za Google na Yahoo! ili watu wanapotafuta habari mbalimbali kwenye mtandao wa tarakilishi waweze kupata blogu yako iwapo ina habari ambayo wanaitafuta. Kusajili google.com bonyeza hapa. Kusajili yahoo.com bonyeza hapa.

Kuna mradi unaoorodhesha blogu za Waafrika uitwao BlogAfrica. Sajili blogu yako kwa kubonyeza hapa.

Mradi wa Global Voices wa Kituo cha Intaneti na Jamii cha Berkman kina ukurasa wa “Wiki” wenye orodha ya blogu zilizopangwa ki-nchi. Kwakuwa ukurasa huo unatumia teknolojia ya “Wiki” mtu yeyote anaweza kuweka blogu katika orodha hiyo. Iwapo umeshindwa kufanya hivyo unaweza kuniandikia, nitaweka blogu yako. Orodha hii ninaitembelea mara kwa mara, kuongeza blogu mpya na kuisafisha iwapo mtu kaongeza blogu kimakosa. Bonyeza hapa uende kwenye ukurasa huo.

Ni muhimu sana pia kuweka viuongo vya blogu za wengine kwenye blogu yako. Sio lazima wawe wanablobu wa Kiswahili au toka Tanzania. Kawaida wanablogu unaoweka viuongo vyao kwenye blogu yako, nao huweka kiungo cha blogu yako kwenye blogu yako na hivyo kupanua wigo wa wasomaji wako. Njia hii ni muhimu sana maana inajenga mtandao na ushirikiano wa wanablogu.

Kuwa na tabia ya kutembelea blogu za wengine na pia kutoa maoni (kwa kutumia anuani ya jina unalotumia kuingia kwenye blogu yako). Baadhi ya watu wanaweza kujua kuwa una blogu kwa kuona anuani ya blogu yako kwenye maoni uliyotoa kwa wengine.

Weka anuani ya blogu yako kwenye anuani yako ya barua pepe. Huduma kama gmail, yahoo mail, n.k. zinakupa mtumiaji uwezo wa kuweka aina ya saini ambayo itatokea katika kila barua pepe unayotuma. Mwisho wa barua yako unapoandika jina lako, ni vyema basi kukawepo na anuani ya blogu yako. Pia kama una kadi za kazi (zimezoeleka kwa jina la business card), weka anuani ya blogu yako.

Iwapo wewe ni mwandishi wa habari, jaribu kumshawishi mhariri wako ili anuani ya blogu yako iwekwe mwisho mwa kila habari uliyoandika au safu yako.

Unaweza pia kuweka kidude cha “feedburner” katika barua zako. Kidude hiki kinaonyesha vichwa vya habari vya mambo uliyoandika katika blogu yako. Mtu akibonyeza juu ya hicho kidude anapelekwa kwenye blogu yako. Soma kuhusu kidude hicho kwa kubonyeza hapa.

Njia nyingine ni kutuma habari kwa watu wote ambao una anuani zao za barua pepe. Tuma barua moja kwa wote ukiwaeleza juu ya blogu yako na pia ukiwataka wawaeleze wengine. Ni vyema kufanya hivi baada ya kuwa umeweka mambo ya kutosha kwenye blogu yako. Usikaribishe watu iwapo umeandika sentensi mbili tu. Tafadhali usisite kuuliza swali lolote au kutaka msaada.

Advertisements

17 Responses to “Jinsi ya kutangaza blogu yako”

 1. KenyaUnlimited Aggregator » Jinsi ya kutangaza blogu yako Says:

  […] Jinsi ya kutangaza blogu yako […]

 2. Elifuraha Steven Says:

  Natumai kuwa u bukheri wa afya njema, naomba nisaidie jinsi ya kufungua blogu.

 3. MADEBENI Says:

  NISAIDIE JINSI YA KUFUNGUA BLOG

 4. mudrk Says:

  nimeipenda naomb muniungie

 5. alexfredy Says:

  KAKA pole kwa majukumu nimepata shida namna ya kutangaza blog kupitia google.com hasa kusumit request/kujisajili google.com,pia nisaidie kuhusu global voices

 6. jeremia meza Says:

  yes a like my website

 7. Fadhili Moperon Says:

  Mzee Tuelimishe Bwana.
  Lakini Juwa Kuwa Jina La Mungu Ni “yehova” Na Karibuni Ataleta Amani Duniani.(zaburi 37:9-12;zaburi83:18).

  I’m Jehovah’s Witness Naishi Mkoa Wa Sud-kivu,wilaya Ya Fizi,kata Ya Mutambala,kijijini Malinde.

  Kaka Nikiweza Kufungua Blog Yangu Au Website,nitasaidia Watu Wengi Wamjue Mungu Wa Kweli Na Yesu Kristo; Na Waijue Vilevile Biblia Ili Waje Kuokolewa(mathayo 24:17;yohana 17:3).

  Kazi Njema Kwako Na Kwenu Wadau Wote.

 8. Gastar Says:

  Habari…? Natumaini kuwa ni mzima wa afya tele hata mm namshukulu mungu mpaka sasa napumua… Kaka mm ninatatizo nimefungua blog na ninazo blog mbili mpaka sasa kwenye website ya blogger.com lakini nimeshindwa kuzitangaza mpaka sasa kwenye mtandao wwte kutokana na kutokuelewa jinsi ya kuzitangaza. Pia niliomba kuweka matangazo ktk hizi blog wakaniletea data lakn pia siwezi jinsi ya kuziingiza hizo data za matangazo ktk blog zangu. Halaf kitu kingine jinsi ya kutangaza hizi blog kuna ghalama zzte zinazohitajika kwa ajili ya matangazo na km zipo hizo ghalama je, ni kiasi gani….? Km hautojali naomba unisaidie coz naitaji kuingia ktk biashara hii na ninamatumaini pia utanijibu haraka iwezekanavyo……!

  Mm wako Gastar.

 9. mikidadi Says:

  Kwaajili ya kuweka picha

 10. Absalom kusaya magibo Says:

  Nisaidie jinsi ya kufungua blog yangu ili niweze kuitumia

 11. mussahassan Says:

  Blogu yangu niliyo omba haifunguki nini nifanye ifunguke na kuweza kuitumia vema

 12. read this Says:

  I know this site offers quality dependent content and
  additional material, is there any other web site which
  provides these things in quality?

 13. Symon tewele Says:

  Asante sana kwa ushauri nimeipenda hii naomba mtembelee na Mimi blog yangu kwa kubofya symontewele. Blogspot.com

 14. edger Says:

  nimepnda kipindi chenu sem naomba msaad nimefungua blog sema nimeshindwa kuweka vitu

 15. SIMON ZABRON Says:

  naomba uniwekee namimi blog yangu kwenye mradi wa blog afrika mi nimeshindwa.
  http://www.musikibongo.blogspot.com

 16. Philemon Ng'hambi Says:

  Reblogged this on mwenyenyumba and commented:
  Fanya yote uikuze blog yako. Kama utafuata njia hizi itakuwa rahisi zaidi kwako kufikia malengo yako.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s


%d bloggers like this: