Kwa sasa maelezo ya jinsi ya kuandika jambo kwenye blogu yako yanahusu huduma ya blogu ya http://blogspot.com ambayo ndio inatumiwa na wengi kwa sasa. Ingawa ina mapungufu yake, bado ina urahisi fulani hasa kwa watu wanaoanza. Baadaye nitaandika maelezo ya huduma nyingine hasa WordPress ambayo ni programu huria. Kwahiyo ili kufuatana nami katika maelezo haya itakupasa ufungue blogu kupitia: http://blogspot.com
Ukishafungua blogu yako, kinachofuata ni kuandika unayotaka. Tembelea blogu za wengine ili kupata picha ya mambo ambayo unaweza kuwa unaandika. Ili uandike jambo, ingia kwenye blogu yako kwa kutumia neno lako la siri. Ukishaingia bonyeza pale pasemapo: New Post (penye alama ya msalaba wa kijani [Tazama mchoro hapo chini]). Ukishabonyeza hapo utapelekwa kwenye sehemu ambayo itakuwa na kisanduku cha kuandika kichwa cha habari yako na pia sehemu ya kuandika unayotaka.
|
|
Blog Name |
New Post |
Change Settings |
Last Update |
Posts |
|
HAPA PATAKUWA NA JINA LA BLOGU YAKO |
05 Feb 2006 | 0 |