Mwezi wa nane mwaka huu niliandika kuhusu huduma ya Wetpaint ambayo inakuwezesha kujenga blogu, wiki, au tovuti yako mwenyewe bila kuwa na haja ya kujua lugha ya kujenga tovuti (HTML au nyinginezo) na pia bila kutakiwa kushusha programu yoyote kwenye kompyuta yako. Huduma kama hizi ni muhimu sana kwa watu walioko katika nchi za Kusini ambapo wengi wanatumia kompyuta ambazo sio zao (kwenye migahawa) hivyo inakuwa vigumu kushusha programu kwenye kompyuta hizo. Pia inakuwa vigumu kutumia muda mrefu kwenye kompyuta kujifunza mambo kama ujenzi wa tovuti toka A hadi Z. Bonyeza hapa usome niliyoandika kuhusu Wetpaint na huduma nyingine.
Sasa kampuni ya incuBeta ina huduma inayofanana kiasi na Wetpaint ambayo inaitwa Synthasite. Huduma hii bado iko kwenye matengenezo ila unaweza kuwapa anuani yako ili wakutaarifu itakapokuwa tayari. Bonyeza hapa.
September 27, 2007 at 12:16 am |
habari yako salama mimi nimefungua hii blogspot kama kujaribu na nilimuuliza kaka yangu michuzi akanifahamisha jinsi ya kufungua na sasa nishafungua inafika miezi 2
October 15, 2007 at 3:23 pm |
nimeon amaelekezo yako namun aya kutegeneza blog,pia na mimi ninapenda kujiunga ili niwe n ablog yangu,laikini ninashidwa
nisaindie ,nifanyeje
August 7, 2009 at 9:31 am |
naomba unipe maelekezo zaidi nianzaje?
December 31, 2009 at 9:11 am |
Nimefungua blog yangu lakini nimeshindwa kujua idadi ya watembeleaji wangu hivyo naomba unisaidie.Nataka nitumie sidebar kwa ajili ya matangazo madogo nimeshindwa naomba msaada pia.Nilikutumia email lakini sijapata jibu hadi leo.Nitashukuru kwa msaada wako.
February 22, 2010 at 10:51 am |
nataka hii iwe tovuti yangu