Kuna zana mpya ambayo itawafaa sana watu wenye nia ya kuwa na tovuti, blogu, au wiki zao wenyewe lakini hawana ujuzi wa utalaamu unaotumika kutengeneza tovuti, blogu, au wiki. Zana hii inaitwa Wetpaint. Kwa dakika chache na bila ujuzi wowote zaidi ya ujuzi wa kutumia tarakilishi, unaweza kuwa na blogu au tovuti yako mwenyewe. Bonyeza hapa ujionee mwenyewe. Majuzi niliandika kuhusu zana hiyo na nyingine zinazofanana katika blogu yangu, bonyeza hapa na hapa ili usome niliyoandika.
September 12, 2006 at 8:55 pm |
Huwa ninapofungua blog yako kwa kweli sichoki kusoma vile vitu adimu ambavyo umekuwa ukitupatia jambo linaloniuma ni kuwa ninajisikia vibaya sana kushindwa kuandika mara kwa mara wakati wewe unatuandikia hata huchoki na wala hukati tamaa.Jambo moja ninalokusisitiza usichoke kutupa vitu hasa sisi tulio kizani baba kaza buti mtu wangu Ndesanjo kwani hilo hata Deogratius Zegge wa Kijenge Mwanama Arusha analitambua hilo.
December 26, 2006 at 10:35 am |
[...] Mwezi wa nane mwaka huu niliandika kuhusu huduma ya Wetpaint ambayo inakuwezesha kujenga blogu, wiki, au tovuti yako mwenyewe bila kuwa na haja ya kujua lugha ya kujenga tovuti (HTML au nyinginezo) na pia bila kutakiwa kushusha programu yoyote kwenye kompyuta yako. Huduma kama hizi ni muhimu sana kwa watu walioko katika nchi za Kusini ambapo wengi wanatumia kompyuta ambazo sio zao (kwenye migahawa) hivyo inakuwa vigumu kushusha programu kwenye kompyuta hizo. Pia inakuwa vigumu kutumia muda mrefu kwenye kompyuta kujifunza mambo kama ujenzi wa tovuti toka A hadi Z. Bonyeza hapa usome niliyoandika kuhusu Wetpaint na huduma nyingine. [...]
June 22, 2007 at 5:16 am |
this is website especially for tanzanian around the world
June 22, 2007 at 5:17 am |
kama una maoni au ushauri unakaribishwa
September 14, 2007 at 8:38 am |
Bw. Ndesanjo, dalasa hili la kufungua tovuti ni zuri mno. Hongera sana.
December 27, 2007 at 6:46 am |
Thank you for your fantastic support. I have made my own website through your support. Thanks once more!!!!!!!!!!!!!!
August 23, 2008 at 2:03 pm |
Nimefurahishwa ka kazi yako ya kutupa darasa na sisi wachanga katika blog, nakuomba unielekeze kuhusiana na kuweka blog za wenzagu katika blog yangu nifanye nini ili niwe na orodha ya blog za wengine
October 30, 2009 at 9:43 pm |
DAAAAAAA,NIMECHELEWA SANA KAKA KUDAKA WEB KAMA HII,UPO JUU MKUBWA……………..ENDELEZA GEM
April 24, 2010 at 5:59 pm |
Mara chache ninazoingia Internet Cafe kotokana n matatizo ya kipato huwa siachi kutembelea blog yako mana najua tu lazima nitapat jambo nisiloliifahamu,napenda sana comment na mawazo yako hata kwenye newspaper natamani nami niwe na blog yangu lakini sijui nianzie wapi
July 14, 2010 at 7:07 am |
Naomba msahada wako. naomba unitumie mwongozo wa jinsi ya kuanza kutengeneza blog .am interested bt i dont know nianzie wapi.
August 20, 2010 at 11:32 pm |
bado tunapigana na blog zetu ili zisimame kazi ipo mikono yenu inahitajika sana,kukosoa na kushauri karibu sana,tunahitaji nguvu kutoka kwenu!!
August 7, 2012 at 11:56 am |
Tafandha ndugu naomba unipe muongozo ili nifugue blogu yangu.natanguliza shukulani zangu kw kunipa msaada uo.
October 30, 2012 at 10:43 am |
thanks Bw.Ndesajo nami pia nimetengeneza website ila naomba unielekeze kuhususiana na ku publish my website kwani naona kama panahitajika hela ili kufanya hivyo
February 23, 2013 at 9:46 am |
zaka